Blog hii ni kiwanja cha wapenzi ndugu jamaa wa Mafumu Bilali Bombenga na African Beat Band. Band hii ilianza mwaka 1998 chini ya uongozi wangu mimi Mafumu Bilali. Mimi hupuliza Saxophone chombo ambacho nimekuwa napuliza kwa miaka 37. Bendi hii hupiga kila aina ya muziki kutokana na experience ya wanamuziki waliopo. Blog hii itakuwa inatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu bendi, kazi zake, wanamuziki wake, wapenzi wake na kadhalika. Usikose kuchungulia, kuuliza maswali na kuchangia kwa mawazo yoyote.